Mar 2, 2014

NDEGE KUBWA KULIKO ZOTE DUNIANI.

   Inaitwa HAV304. Imetengenezwa na kampuni inayoitwa Hybrid Air Vehicles. Inaweza kukaa angani kwa muda wa wiki 3 na nusu. Itauzwa kwa bei ya paundi millioni 30. Itaweza kubeba abiria 50 na tani 50 (kilogramu 50,000) za mzigo.

  Itakuwa na uwezo wa kutua kwenye barafu, kwenye maji na nchi kavu. Itakuwa na sehemu za helicopter na ndege ya abiria ya kawaida.
Hivyo haitahitaji uwanja wa ndege ili kutua.

  Baadhi ya kampuni za ndege zimeonesha kwamba zinataka ndege hiyo, lakini bado haijapata wateja wengi.

Mambo yakienda sawa, hii ndiyo itakuwa ndege kubwa zaidi duniani. Kwa sasa, ndege aina ya Airbus A380-800 ndiyo ndege kubwa zaidi duniani. Ina uwezo wa kubeba aibiria zaidi ya 250!

Jan 24, 2014

FANTASTIC INSPIRATIONS.


 HeLLO.
   Leo tuangalie baadhi ya wanawake ambao wanastahili pongezi kwa kudhubutu na kuweza katika Aviation industry.
  Wafuatao ni vijana na wanawake ambao ni marubani na marubani wazoefu (Captains) katika Afrika, ambao ninafikiri wanatakiwa kutambulika.


1. Neema Swai (First Officer Precision Air Tanzania).  
Amekaa katikati.
Anaendesha ndege aina ya ATR 42-600.
2. Esther Mbabazi. (First Officer RwandAir).
   Ni Rubani wa kwanza wa Kike nchini Rwanda.
   Baba yake pia alikuwa rubani, lakini alikufa 
  kwenye aksidenti mbaya ya ndege nchini Rwanda
  kati ya miaka ya 1995-1998. 
Anaendesha ndege aina ya Embraer 190.
 3. Abimbola Jayeola. (First female Commercial Helicopter Pilot Nigeria).

4. Tonika Johnson. (Captain Arik Airlines, Lagos, Nigeria).

5. Amsale Gualu. (First Female Captain Ethiopian airlines, Ethiopia).
Anaendesha ndege aina ya Bombardier Q400.

6.Irene Mutungi. (Captain Kenya Airways).
Anaendesha ndege aina ya Boeing 767.
7. Imoleayo Adebule, 23. (First Officer Aero Contractors, Nigeria).

8. Milcah Mumbe, 21. (First Officer Safarilink, Kenya).
Anaendesha ndege aina za Cessna Caravan.
9. Cecylia Gellejah, 23. (First Officer Flightlink Air Charters, Dar es Salaam).


Mar 15, 2013

BOEING 787 THE DREAMLINER KURUDI KAZINI.

The Dreamliner!
    Kampuni ya kutengeneza ndege za kibiashara ya Boeing,ilipata kibali cha kufanya safari za majaribio kwa ajili ya ndege yao mpya ya Boeing 787 The Dreamliner juzi tarehe 13 kutoka FAA (Federal Aviation Administration) Marekani. Kibali hicho kinakuja baada ya kampuni ya Boeing kutoa designs za betri mpya amabazo zitatumiwa na ndege aina ya Boeing 787.
   FAA iliamuru mashirika yote duniani yaliuyokuwa yakitumia ndege hizo tarehe 2 Januari mwaka huu,baada ya ndege ya shirika la Japan Airlines kupata dharura ikiwa angani. Dharura hiyo ilihusisha betri ya Auxiliary Power Unit kuungua na kuanza kutoa moshi amabo uliingia kwenye chumba cha abiria.
   Boeing imerusha ndege ya kwanza leo katika uwanja wa ndege wa Narita karibu na Tokyo Japan (kama ionekanavyo kwenye picha chini).
Ndege aina ya Boeing 787 ikiwa katika uwanja wa Narita Tokyo kabla ya majaribio.
(Credit:ANA)
   Boeing itakuwa kampuni ya kwanza kutumia betri za aina ya Lithium-ion,ambazo zinatunza zaidi charge kwa muda muda mrefu kuliko aina zingine na zinatumika kwa muda mrefu. Kila betri moja ina seli nane ili kuhakikisha usalama zaidi!
   Pia,zimetengenezwa na kuta maalumu kwa ajili ya kuzuia moto (fireproof shell) au joto la betri moja lisiathiri seli nyingine. Kama majaribio hayo yatafanikiwa,ndege hizo zitarudi kazini ndani ya wiki chache baada ya leo!


Mar 7, 2013

CONDENSATION TRAILS

Emirates Airbus A380-800
 
Umewahi kuona moshi mrefu unaoachwa na ndege angani? Bila shaka umeshawahi kuona kitu kama hicho,kama bado basi naamini umeshaoona kutoka kwenye picha hapo juu! Teh teh!
  Huenda pia umejiuliza nini chanzo cha huo moshi! Leo nimejaribu kutafuta habari kuhusu mada hiyo na haya ndiyo niliyoyapata!

  Hali (tabia) hiyo inaitwa Contrail (Condensation Trail) yaani moshi mrefu ulioganda. Mara nyingi utaona moshi huo nyuma ya ndege au juu ya eneo la mabawa ya ndege au hata kwenye sehemu ya mwisho ya bawa  la ndege (wingtip). Kutegemeana na joto-ridi (temperature) katika anga za juu,moshi huo unaweza  kudumu kwa kipindi fulani (dakika chache) au hata kwa masaa na kusambaa kisha kuwa kama mawingu!
  Moshi unaodumu kwa muda mrefu,unakisiwa kuwa ni moja kati ya vyanzo vikubwa vya kubadilika kwa hali ya hewa duniani (Global climate change).
  Sasa wacha tuone nini chanzo cha moshi huo unaoganda baada ya ndege kupita katika sehemu fulani ya anga.

  KUGANDA KWA HEWA.

  Zao kubwa la mafuta yanayochomwa na injini za ndege ni hewa ya Carbon dioxide na mvuke wa moto (water vapour). Katika anga za juu sana (8,000 meters),ambako kuna hewa nyepesi na isiyo na umaji-maji  (humidity) mvuke huo wa moto unaotoka kwenye injini za ndege unaweza kuganda! 
  Kuelewa hilo,fikiria mfano huu.............
(Umechemsha maji,na yamepata joto kali! Halafu ukayaweka kwenye jokofu {deep freezer}. Kumbuka maji yaliyo kwenye chupa ni ya moto,lakini hewa inayozunguka chupa hiyo ni baridi sana. Hivyo,maji yaliyo ndani ya chupa lazima yatakuwa baridi na kuganda).
  Ndivyo ilivyo kwa mvuke wa moto unaotoka kwenye injini za ndege ikiwa anga za juu sana. Lakini,kuna sababu zinazochangia mvuke huo kuganda...Zifuatazo ndizo sababu chache zinachochangia mvuke huo wa moto kuganda!

1.JOTO-RIDI (TEMPERATURE).
~Kama nilivyoeleza kwenye makala zilizotangulia kuhusu hewa iliyo huko juu kuwa ni nyepesi na haina unyevu-nyevu. Hivyo hewa (mvuke) wa moto unaotoka kwenye ndege ukikutana na hewa hiyo ya baridi lazima igande. Lakini hilo litawezekana tu ikiwa joto-ridi la hewa inayozunguka ni  chini ya nyuzi-joto -40 (-40 degrees of centigrade).

2.KUPUNGUA KWA MGANDAMIZO WA HEWA (AIR PRESSURE).
 ~Kipindi mabawa ya ndege yanatengeneza nguvu inayoitwa Lift inayofanya ndege iache ardhi na kupaa,kunakuwa na hewa inayozunguka kama duara kwenye sehemu ya mwisho ya bawa la ndege (wingtip) Hali hiyo inaitwa Wingtip Vortex . Angalia picha...
Singapore Airlines Airbus A380-800 Landing
  ~Hii inasababishwa na nguvu-kani nyingine ya asili iitwayo Drag inayotengenezwa na ndege yenyewe inapoenda mbele. Mambo kama spidi,hali ya hewa na ,mengineyo yanatiliwa sana mkazo katika safari ili kuzuia moshi huo ulioganda kutokea.
  Kwa habari zaidi kuhusu wingtip vortices,soma hapa  http://en.wikipedia.org/wiki/Wingtip_vortices

Feb 11, 2013

GPS (GLOBAL POSITIONING SYSTEM).

  Huenda umekuwa ukijiuliza mara kadhaa kuhusu jinsi kifaa hiki kinafanaya kazi. Hapa utapata kujua kila kitu kuhusu GPS kwa njia na lugha rahisi zaidi.

  GPS (Global Positioning System) NI NINI?

  Ni mfumo unaotumika kukokotoa mahali mtu au kitu au kifaa hicho kipo kwenye sehemu yoyote duniani. Mfumo huo unaongozwa na kitengo cha Ulinzi cha Marekani (DoD US Department of Defense) na Shirika la anga  NAVSTAR (Navigation Satellite Timing and Ranging).
  Mfumo huo unatumia satellite zilizo angani zinazozunguka dunia katika umbali wa kilomita 299,460 kutoka usawa wa bahari katika mwendo-kasi ya kilomita 11,270 kwa saa (spidi ambayo ni mara 10 ya spidi ya ndege ya abiria iendayo kasi zaidi duniani Cessna Citation X). Satellite hizo hutumia masaa 12 kumaliza mzunguko wazo. Hii inamaanisha kwamba,satellite hizo hupita katika eneo lolote duniani mara mbili kwa siku.
  Mfumo huo wa GPS una vitengo vitatu...

   1.MFUMO WA SATELLITE WENYEWE ANGANI (GPS Constellation).
 ~Kitengo hiki ndio satellite zilizo angani ambazo kwa mara ya kwanza ziliwekwa mwaka 1978 na shirika la Air Force la Marekani. Mpaka sasa kuna satellite 24 hivi angani zinazozunguka dunia katika mwendo-kasi wa kilomita 11,270. Zimewekwa mbali na dunia ili kuhakikisha kuwa haziathiriwi na hali ya hewa ya dunia.
  Zinaendeshwa na nguvu ya jua,na betri za Nicad kwa dharura kama ikitokea Kupatwa kwa jua. Pia ndani yake kuna saa za ki-atomiki nne ambazo ziko sahihi sana,lakini ni moja tu ndiyo inayotumika.

  Njia za satellite (Satellite Orbit)

 ~Kuna njia kuu sita ambazo satellite hizo 24 zinatumia kuzunguka dunia. Hii ikimaanisha kwamba Katika kila njia ya satellite hizo kuna satellite 4 zinazioitumia njia hiyo (ukigawanya 24 kwa 4). Kama ionekanavyo kwenye picha chini 
  

Mawimbi ya Satellite (Satellite Signal)

 ~Mawimbi ya redio ya Satellite za GPS yanatumia masafa (frequency) ya aina mbili kufikisha taarifa duniani katika mwendo-kasi wa mwanga kilomita 299,460 kwa saa (186,000 miles per hour). Masafa hayo yanaitwa L1 na L2. Masafa hayo yanatumia muda ambao ni chini ya sekunde moja kufika duniani kutoka katika satellite hizo. 
  Mawimbi hayo yanahitaji kusafiri moja kwa moja toka kwenye satellite hizo bila kizuizi chochote njiani. Hii inamaanisha kwamba,mawimbi hayo hayawezi kupenya katika udongo,misitu minene au kuta mbalimbali.

2.KITENGO/KITUO CHA UONGOZAJI (DoD Monitoring).
~Hiki ni kitengo cha uongozaji Falcon Air Force Base kilicho nchini Marekani katika mji wa Colorado Spring. Kuna vituo vingine katika nchi ya Hawaii,kisiwa cha Ascension,Diego Garcia na Kwajelein. Vituo hivyo vinaongoza satellite hizo na kama kuna tofauti zozote kwenye njia za satellite hizo,kitarakirishi (computer) katika vituo hivyo hutuma habari hizo katika satellite ili kurekebisha tatizo hilo.

3.KITENGO CHA MTUMIAJI (User Segment).
~Hiki ndicho kitengo kinacho kamilisha mfumo wa GPS yaani Mtumiaji. Baada ya mawimbi hayo kutoka katika satellite,yanakuja moja-kwa-moja kwa mtumiaji ili yaweze kutafsiriwa na kupata majibu. Hapa kuna watumiaji wawili (Wanajeshi na raia wa kawaida). Wanajeshi wana teknolojia kubwa zaidi ya ile ipatikanayo katika GPS za raia wa kawaida. Hii ni kwa sababu,wanajeshi wanahitaji vifaa sahihi zaidi kwa ajili ya matumizi yao.

   ~Sasa,acha tuone jinsi kifaa hiki kinaweza kukokotoa mahali ulipo kwa usahihi kabisa!

KUKOKOTOA UMBALI KATI YA GPS DUNIANI NA SATELLITE!

   Ili Kifaa-kipokeaji cha mawimbi yaani GPS Receiver kilicho duniani kiweze kukokotoa mahali ulipo kwa usahihi kabisa,kinahitaji kwanza kujua umbali uliopo kati yake na Satellite za GPS. Kinafanya hivyo kwa kupima muda ambao mawimbi hayo kutoka kwenye satellite yametumia kukifikia. 
  Kitendo hicho kinaitwa Satellite Ranging. Kinachofanyika ni kwamba,satellite ya GPS inatuma mawimbi yake kuja katika kifaa-kipokeaji cha GPS kilicho duniani. GPS iliyopo duniani inakokotoa muda ambao mawimbi yaliyotumwa na Satellite umechukua kukifikia kwa kutumia saa ya ki-atomiki iliyo ndani yake.
  ~Lakini,GPS iliyo duniani inawezaje kujua muda ambao mawimbi hayo yaliondoka kwenye satellite iliyo angani?
Kitu rahisi sana!!!!

  GPS zote,zimeunganishwa (synchronized) na satellite ili ziweze kutengeneza code fulani katika wakati mmoja ili kurekodi kila kazi inayofanywa na satellite pamoja nazo. Hivyo,GPS iliyopo duniani itafungua code hiyo na kukumbuka mawimbi hayo yalitumwa saa ngapi. 
  Sasa inaweza kukokotoa muda ambao mawimbi hayo yalitumia kufika duniani. 
  ~Lakini,muda huo sio umbali. Sasa kifaa hicho kinapataje umbali? Endelea kusoma...

  Kinachofanya ni kuzidisha muda huo na mwendo-kasi wa Mwanga (299,460 km kwa saa) ili kupata umbali ambao mawimbi hayo yametumia kufika duniani!

KUKOKOTOA ENEO ULILOPO!
  Sasa,GPS inajua umbali uliopo kati yake na satellite hatua inayofuata ni kukokotoa mahali ulipo. Hapa kuna mahesabu yanayochanganya kidogo,lakini nitajaribu kurahisisha.
  Fikiria mfano huu..... 
Umepotea nchini Marekani na hujui pa kuanzia. Halafu anatokea mtu anakwambia 'upo umbali wa Maili 625 (1,006.25 km) toka mji unaitwa Boise. 

Unaweza kuchanganyikiwa kidogo,kwa sababu ukichora duara kama hilo, unaweza kuwa upande wowote kutoka Boise. Lakini anatokea mwangine anakwambia 'upo umbali wa Maili 690 (1,110.09 km) kutoka mji wa Minneapolis'.
  Sasa,unapata kitu fulani. Ukichora maduara mawili unaweza kukisia kwamba "huenda niko sehemu fulani kati ya maduara hayo mawili,huenda pale ambapo yanakutana". 
  Lakini,akitokea mwingine akakwambia "upo umbali wa maili 620 (998 km) toka Tucson Arizona" sasa utajua mahali hususa ulipo!
Utaangalia pale ambapo maduara yote matatu yamekutana,na sasa utakuwa umejua mahali ulipo kwa hakika. Likiongezeka duara lingine, utapata habari sahihi zaidi! 

  ~Hivyo ndivyo mfumo wa GPS unafanya kazi kukupa habari kuhusu mahali ulipo. Kifaa chako cha mkononi,kinahitaji mawimbi ya satellite angalau tatu ili kuwa sahihi zaidi.
 Kinapopokea mawimbi ya satellite ya kwanza,kinajifunga ili kukokotoa umbali kati yake na hiyo satellite na kupata ni kilomita 299,460 (12,000 miles) kuzunguka satellite hiyo. Hapo hakitoi taarifa sahihi kwamba uko wapi,lakini kinasema upo mahali fulani kuzunguka hilo duara (Duara hilo huchorwa kuzunguka satellite angani na si duniani).
  Baada ya kumaliza katika satellite ya kwanza,kinajifungua na kupokea mawimbi ya satellite nyingine na kufanya kile ambacho kilifanyika kwa ile ya kwanza..kinafanya hivyo kwa satellite nyingine zote tatu au zaidi.
  GPS iliyo duniani inapopata pointi ambayo maduara yote matatu yamekutana,inanakili Longitude na Latitude za eneo hilo na kukupa taarifa kwamba upo mahali fulani.

  Yote hayo yanafanyika kwa muda mfupi sana ikiwa sehemu ulipo hakuna vizuizi vingi kama vile kuta,milima na kadhalika.    

Feb 8, 2013

INJINI YA NDEGE (JET ENGINE) INAFANYA KAZI.JINSI GANI?

   ~Bila shaka umewahi kujiuliza 'injini ya ndege za abiria inafanyaje kazi?!' Na huenda hukupata majibu!
 Ukiendelea kusoma,utapata jibu la swali hilo! Kwanza,hebu tuone sehemu za injini ya ndege.

   ~Zifuatazo ni sehemu kuu tano za injini ya ndege (Jet Engine)!
1.KIIGIZA-HEWA (Air inlet) 
  ~Hii ni sehemu ya mbele kabisa ya injini ambayo inakusanya hewa na kuiingiza katika sehemu inayofuata (inayoitwa Engine Air compressor (Kigandamizi-hewa).

2.KIGANDAMIZI-HEWA (Engine Air Compressor).
  ~Sehemu hii ina kazi ya kugandamiza hewa iliyoingizwa na kiingizi--hewa. Hewa inapogandamizwa,pressure inaongezeka. Na pressure inapoongezeka,spidi ya hewa hiyo huongezeka. Kwa hiyo sehemu hii,inafanya kazi ya kuongeza mwendo-kasi wa hewa inayoingia kwenye injini ya ndege. Baada ya kukamilisha kazi hiyo,kazi nyingine ni kuielekeza hewa hiyo kwenye sehemu ya tatu ya injini ya ndege.

3.JIKO LA INJINI (COMBUSTION CHAMBER).
  ~Hapa ndipo nguvu inayoendesha ndege inatengenezwa. Ni sehemu ambayo hewa iliyo chini ya mgandamizo na mafuta vinakutana.
 Kama uonavyo kwenye picha,kuna viji-bomba vodogo vinavyoleta mafuta kwenye injini kutoka kwenye mabawa ya ndege (airplane wings) au sehemu nyingine inayotunza mafuta kwenye ndege (lakini,mchanganyiko huo tu wa mafuta na hewa iliyo chini ya mgandamizo,ndio utatengeneza nguvu ya kuendesha ndege??).
   Pia,kuna plagi za cheche (spark plugs) zinazochochea mchanganyiko huo wa mafuta na hewa na kuwasha moto mkubwa/gesi zilizo moto sana (zilizo katika chumba kidogo lakini).
  Gesi hizo zilizo chini ya mgandamizo mkubwa,zinaelekezwa kwenye sehemu nyingine tena ya nne ambayo,huelekeza gesi hizo zilizo na pressure kwenye sehemu inaitwa Turbine.
  Sehemu hii ina mapanga/vitu kama feni vinavyozunguka kwa kasi sana ili kuongeza spidi/mwendo-kasi wa gesi hizo za moto.
  Sehemu hiyo inatuleta katika sehemu ya tano ya injini inayoitwa Nozzle.

4.NOZZLE.
   ~Hapa,gesi hiyo inayosafiri kwa kasi sana,inanyooshwa (directed) kwenda sehemu ya  mwisho ya nijini ya ndege ambayo inapeleka gesi hizo za moto nje ya ndege kwa kasi kubwa sana.

5.EXHAUST.
  ~Hapa ndipo gesi hizo hutolewa nje kabisa ya injini ya ndege baada ya kupita sehenu zote nne za mwanzo!
  

Feb 4, 2013

UWANJA WA NDEGE HATARI ZAIDI KUTUA DUNIANI!

    Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Paro (IATA:PBH, ICAO:VQPR) ulio nchini Bhutan katika milima ya Himalayas,ndiyo uwanja unaofikiriwa kuwa uwanja hatari zaidi duniani kwa ndege kutua na kuruka. Uwanja huo,upo kilomita 6 hivi toka mji wa Paro kwenye bonde la ufa la mto Paro Chhu.
    Uwanja huo una barabara ya kurukia ndege na kutua (Runway 15/33) moja yenye urefu wa futi 6,445 (1,964 m) urefu ambao unalingana na viwanja vya mpira wa miguu 21 vyenye urefu wa mita 120 (393.6 ft),moja kati ya barabara za ndege kurukia na kutua fupi sana duniani. Una jengo moja la abiria lenye check-in counters 4,geti moja la kuingilia kwenye ndege na jengo la mizigo.
   
    KWA NINI NI HATARI ZAIDI?
Sababu za uwanja huo kuwa hatari zaidi duniani.
   1. MILIMA MIREFU SANA ILIYOUZUNGUKA UWANJA. Uwanja huo umezungukwa na milima ya Himalayas yenye urefu wa zaidi ya futi 18,000 (5,487 m),urefu ambao unakaribia ule wa mlima Kilimanjaro. Hebu fikiria urefu wa mlima kilimanjaro,halafu piga picha sehemu iliyozungukwa na milima kama hiyo pande zote!
   2.BARABARA FUPI YA KURUKIA NDEGE (RUNWAY). Barabara yenye urefu wa futi 6,445 tu. Runway kwenye viwanja vingi vya ndege duniani zina urefu wa kuanzia futi 10,000 (3,048 m) hivi. Hilo linafanya ndege kubwa kutoweza kutua.
   3.PEPO KALI ZINAZOVUMA KUTOKA KWENYE MTO.
Sehemu yoyote yenye vyanzo vya maji kama mito na maziwa,kunakuwa na pepo kali zinazovuma kuelekea nchi kavu. Uwanja huo wa ndege umepakana na mto uliotengenezwa na bonde la ufa la mto Paro Chhu. Unaweza kuona jinsi kunakuwa na upepo mkali eneo hilo.

   Ni Mashirika machache sana ya ndege yanayoutumia uwanja huo. Baadhi yao ni Budha Air, Druk Air na Tashi Air. Ni marubani nane tu duniani mpaka sasa ambao wameruhusiwa kutua katika uwanja huo. Shughuli zote za uwanja huo hufanywa mchana wakati kuna mwanga,na hakuna ndege inaruhusiwa kutua usiku au kukiwa na hali mbaya ya hewa.

~Zaidi ya huo,kuna viwanja vingine hatari kama vile Kansai International airport,Princess Juliana International airport na Madeira Airport.

Feb 2, 2013

HEWA UNAYOVUTA NDANI YA NDEGE INATOKA WAPI?


Wengi wamekuwa wakijiuliza 'Hewa tunayovuta ndani ya ndege inatoka wapi ikiwa,katika anga ambayo ndege hii inatembea kuna oksijeni kidogo?'

  Kwanza,kuna kitu watu wengi wameelewa vibaya kuhusu upungufu wa oksijeni katika anga za juu....
SI KWELI KWAMBA OKSIJENI HUISHA NDEGE AU ROKETI INAPOPANDA JUU, NA NDIO MAAANA MFUMO WA KUTENGENEZA OKSIJENI NDANI YA NDEGE UNAHITAJIKA!!!
  Kianchobadilika/kupungua ni mgandamizo wa hewa ya oksijeni (air pressure) na hilo hufanya iwe vigumu kwa mtu kupumua.

  Hewa tunayovuta juu ya ardhi ina mgandamizo na unyevu-nyevu mkubwa na hii inasaidia pia kuweka mapafu na njia za hewa katika hali salama...kwa nini?
  Ni kwa sababu katika matundu ya pua kuna ute-ute uitwao Mucus,unaosaidia kunasa bacteria na kuwazuia
kuingia katika miili yetu na kusababisha magonjwa.
  Hewa iliyopo ndani ya ndege ni kavu na nyepesi,kwa sababu ipo chini ya mgandamizo (pressure) lakini haina unyevu-nyevu.
   Hii ni kwa sababu hewa hiyo INATOKA KWENYE INJINI ZA NDEGE!



  Kama ulisoma makala katika ukurasa wa blog hii kwenye Facebook http://facebook.com/Runway29R
uliona jinsi injini ya ndege inavyofanya kazi. Kwenye sahemu ya injini ambayo inagandamiza hewa (engine compressor) na kuipeleka kwenye sahemu ya kuchanganya mafuta na hewa na kuchoma mchanganyiko huo na kutengeneza nguvu,ndipo hewa inayotumiwa na abiria inapotoka.
  Kutoka huko,kuna mfumo unaitwa Bleed Air system unaochukua hewa kutoka kwenye injini na kuuingiza kwenye chumba cha abiria.
  Unakumbuka tulisema hewa iliyopo ndani ya ndege haina unyevu-nyevu na ni kavu? Na pia jinsi hewa tunayovuta ardhini (yenye unyevu-nyevu) inavyotusaidia kujikinga na magonjwa?
  Kama unakumbuka,unaweza kujiuliza "Si ni rahisi sasa kama kuna abiria ana ugonjwa unaoambukizwa kwa  njia ya hewa,kuwaambukiza abiria wengine?"

  Jambo hilo limetiliwa mkazo sana na mainjinia wa ndege na ndio maana wametengeneza mifumo ya kuua vijidudu vya magonjwa. Wametengeneza mfumo ambao unaosafisha hewa ndani ya ndege kabla hata ya hewa hiyo kukufikia abiria. Juu ya kila kichwa cha abiria au kwenye miguu,kuna button mbalimbali pamoja na tundu lenye kitu kama nyavu. Linaitwa AIRCRAFT CABIN AIR FILTER.
  Ndani ya tundu hilo kuna huo mfumo unaosafisha hewa kabla ya kuja kwa mtumiaji/abiria kama ionekanavyo kwenye picha...
 Hivyo,usiwe na wasiwasi kwamba unaweza kupata magonjwa yoyote ukiwa ndani ya ndege.. Ni Salama Sana.

Feb 1, 2013

TAA ZILIZO PEMBENI MWA BARABARA YA KURUKIA NA KUTUA NDEGE..ZINAMAANISHA NINI?

Bila shaka umewahi kuona taa zilizo pembeni mwa barabara
inayotumiwa na ndege kuruka na kutua,sivyo! Umewahi kujiuliza zina kazi gani!
Huenda ulisema "ni kwa ajili ya kumsaidia rubani kuona
mahali ndege yake inatakiwa kutua".

Lakini,taa hizo zina kazi nyingine ya maana sana....!
Ungependa kujua ni nini? Endelea kusoma.

Ndege inapoanza kushuka,inashuka ikiwa na pua yake
(nose) imeanglia chini Lakini katika Angle fulani ambayo
mara zote ni nyuzi tatu (3 degrees).
Taa hizo zinamsaidia rubani kutambua ikiwa ndege yake
inashuka katika angle hiyo inayotakiwa.
Taa hizo zimeundwa kutoa mwanga wa rangi fulani kutokana
na angle ambayo zinaangaliwa.
Zikiangaliwa toka juu sana zinaonekana nyekundu,zikiangaliwa
toka chini kidogo zinaonekana kijani na zikiangaliwa nusu wima(45 Degrees)
zinaonekana nyeupe.

Sasa hebu tuone zinamsaidiaje rubani kujua hilo.

Kanuni ifuatayo inatumika na marubani kujua ikiwa ndege inashuka
katika angle sahihi...

White-white-white-white(yaani upande mmoja nyeupe na wa pili nyeupe)
    ~Ndege ipo kwenye angle sahihi.
White-white-white-red(yaani upande mmoja mbili nyeupe na wa pili nyeupe na nyekundu)
    ~Ndege ipo juu kidogo ya angle sahihi.
White-white-red-red(upande mmoja mbili nyeupe na wa pili mbili nyekundu)
    ~Ndege ipo chini kidogo ya angle sahihi.
Red-red-red-red (pande zote mbili nyekundu)
    ~Ndege ipo chini sana.

FLY EMIRATES WABADILISHA NDEGE INAYOKUJA DAR ES SALAAM!

Leo ni siku nzuri sana kwa wasafiri waendao Dubai. Shirika la ndege la Umoja wa nchi za Kiarabu (UAE-United Arab Emirates) Fly Emirates,limeanza rasmi kutumia ndege yake aina ya Boeing 777-300ER (Extended Range) kwa safari za kutoka Dar es Salaam kwenda Dubai.
Hapo mwanza ilitumika ndege aina ya Airbus A340-500 yenye uwezo wa kubeba abiria 340.
Ndege hiyo mpya ya Boeing 777-300ER itaweza kubeba abiria 360,abiria 8 katika daraja la kwanza (first class) 24 daraja la kibiashara (business class) na 310 daraja la chini (economy class).
Pia itabeba tani 46 za mizigo.

NAULI ZA SAFARI HIYO
Daraja la chini (economy class) kwenda na kurudi-630$

Daraja la kibiashara (business class) kwenda na kurudi-2,260$.

Ndege hiyo itakuwa ikiondoks Uwanja wa ndege wa Dubai saa 1015hrs na kufika Dar es Salaam saa 1455hrs. Na itaondoka Dar es Salaam saa 1645hrs na kufika Dubai saa 2320hrs
http://www.ippmedia.com/frontend/index.php?l=50513