Feb 8, 2013

INJINI YA NDEGE (JET ENGINE) INAFANYA KAZI.JINSI GANI?

   ~Bila shaka umewahi kujiuliza 'injini ya ndege za abiria inafanyaje kazi?!' Na huenda hukupata majibu!
 Ukiendelea kusoma,utapata jibu la swali hilo! Kwanza,hebu tuone sehemu za injini ya ndege.

   ~Zifuatazo ni sehemu kuu tano za injini ya ndege (Jet Engine)!
1.KIIGIZA-HEWA (Air inlet) 
  ~Hii ni sehemu ya mbele kabisa ya injini ambayo inakusanya hewa na kuiingiza katika sehemu inayofuata (inayoitwa Engine Air compressor (Kigandamizi-hewa).

2.KIGANDAMIZI-HEWA (Engine Air Compressor).
  ~Sehemu hii ina kazi ya kugandamiza hewa iliyoingizwa na kiingizi--hewa. Hewa inapogandamizwa,pressure inaongezeka. Na pressure inapoongezeka,spidi ya hewa hiyo huongezeka. Kwa hiyo sehemu hii,inafanya kazi ya kuongeza mwendo-kasi wa hewa inayoingia kwenye injini ya ndege. Baada ya kukamilisha kazi hiyo,kazi nyingine ni kuielekeza hewa hiyo kwenye sehemu ya tatu ya injini ya ndege.

3.JIKO LA INJINI (COMBUSTION CHAMBER).
  ~Hapa ndipo nguvu inayoendesha ndege inatengenezwa. Ni sehemu ambayo hewa iliyo chini ya mgandamizo na mafuta vinakutana.
 Kama uonavyo kwenye picha,kuna viji-bomba vodogo vinavyoleta mafuta kwenye injini kutoka kwenye mabawa ya ndege (airplane wings) au sehemu nyingine inayotunza mafuta kwenye ndege (lakini,mchanganyiko huo tu wa mafuta na hewa iliyo chini ya mgandamizo,ndio utatengeneza nguvu ya kuendesha ndege??).
   Pia,kuna plagi za cheche (spark plugs) zinazochochea mchanganyiko huo wa mafuta na hewa na kuwasha moto mkubwa/gesi zilizo moto sana (zilizo katika chumba kidogo lakini).
  Gesi hizo zilizo chini ya mgandamizo mkubwa,zinaelekezwa kwenye sehemu nyingine tena ya nne ambayo,huelekeza gesi hizo zilizo na pressure kwenye sehemu inaitwa Turbine.
  Sehemu hii ina mapanga/vitu kama feni vinavyozunguka kwa kasi sana ili kuongeza spidi/mwendo-kasi wa gesi hizo za moto.
  Sehemu hiyo inatuleta katika sehemu ya tano ya injini inayoitwa Nozzle.

4.NOZZLE.
   ~Hapa,gesi hiyo inayosafiri kwa kasi sana,inanyooshwa (directed) kwenda sehemu ya  mwisho ya nijini ya ndege ambayo inapeleka gesi hizo za moto nje ya ndege kwa kasi kubwa sana.

5.EXHAUST.
  ~Hapa ndipo gesi hizo hutolewa nje kabisa ya injini ya ndege baada ya kupita sehenu zote nne za mwanzo!
  

4 comments:

  1. Hili somo bado alijakaa vizuri . Inamaana ingine ya ndege haina brock wala piston wala valvu umeshindwa kueleza kitaaram

    ReplyDelete
  2. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  3. unaposema jiko la ingine unamaana gani. @ Ingine inatumiajiko na ilojiko la ingine kitaalam linaitwaje. Pia naomba utusaidie utofauti wa Ingine ya hedkopter na ndege na ya gari kwa kitaaram. Usitumie rafudhi katuni

    ReplyDelete