Emirates Airbus A380-800 |
Umewahi kuona moshi mrefu unaoachwa na ndege angani? Bila shaka umeshawahi kuona kitu kama hicho,kama bado basi naamini umeshaoona kutoka kwenye picha hapo juu! Teh teh!
Huenda pia umejiuliza nini chanzo cha huo moshi! Leo nimejaribu kutafuta habari kuhusu mada hiyo na haya ndiyo niliyoyapata!
Hali (tabia) hiyo inaitwa Contrail (Condensation Trail) yaani moshi mrefu ulioganda. Mara nyingi utaona moshi huo nyuma ya ndege au juu ya eneo la mabawa ya ndege au hata kwenye sehemu ya mwisho ya bawa la ndege (wingtip). Kutegemeana na joto-ridi (temperature) katika anga za juu,moshi huo unaweza kudumu kwa kipindi fulani (dakika chache) au hata kwa masaa na kusambaa kisha kuwa kama mawingu!
Moshi unaodumu kwa muda mrefu,unakisiwa kuwa ni moja kati ya vyanzo vikubwa vya kubadilika kwa hali ya hewa duniani (Global climate change).
Sasa wacha tuone nini chanzo cha moshi huo unaoganda baada ya ndege kupita katika sehemu fulani ya anga.
KUGANDA KWA HEWA.
Zao kubwa la mafuta yanayochomwa na injini za ndege ni hewa ya Carbon dioxide na mvuke wa moto (water vapour). Katika anga za juu sana (8,000 meters),ambako kuna hewa nyepesi na isiyo na umaji-maji (humidity) mvuke huo wa moto unaotoka kwenye injini za ndege unaweza kuganda!
Kuelewa hilo,fikiria mfano huu.............
(Umechemsha maji,na yamepata joto kali! Halafu ukayaweka kwenye jokofu {deep freezer}. Kumbuka maji yaliyo kwenye chupa ni ya moto,lakini hewa inayozunguka chupa hiyo ni baridi sana. Hivyo,maji yaliyo ndani ya chupa lazima yatakuwa baridi na kuganda).
Ndivyo ilivyo kwa mvuke wa moto unaotoka kwenye injini za ndege ikiwa anga za juu sana. Lakini,kuna sababu zinazochangia mvuke huo kuganda...Zifuatazo ndizo sababu chache zinachochangia mvuke huo wa moto kuganda!
1.JOTO-RIDI (TEMPERATURE).
~Kama nilivyoeleza kwenye makala zilizotangulia kuhusu hewa iliyo huko juu kuwa ni nyepesi na haina unyevu-nyevu. Hivyo hewa (mvuke) wa moto unaotoka kwenye ndege ukikutana na hewa hiyo ya baridi lazima igande. Lakini hilo litawezekana tu ikiwa joto-ridi la hewa inayozunguka ni chini ya nyuzi-joto -40 (-40 degrees of centigrade).
2.KUPUNGUA KWA MGANDAMIZO WA HEWA (AIR PRESSURE).
~Kipindi mabawa ya ndege yanatengeneza nguvu inayoitwa Lift inayofanya ndege iache ardhi na kupaa,kunakuwa na hewa inayozunguka kama duara kwenye sehemu ya mwisho ya bawa la ndege (wingtip) Hali hiyo inaitwa Wingtip Vortex . Angalia picha...
Singapore Airlines Airbus A380-800 Landing |
~Hii inasababishwa na nguvu-kani nyingine ya asili iitwayo Drag inayotengenezwa na ndege yenyewe inapoenda mbele. Mambo kama spidi,hali ya hewa na ,mengineyo yanatiliwa sana mkazo katika safari ili kuzuia moshi huo ulioganda kutokea.
Kwa habari zaidi kuhusu wingtip vortices,soma hapa http://en.wikipedia.org/wiki/Wingtip_vortices
No comments:
Post a Comment