Wengi wamekuwa wakijiuliza 'Hewa tunayovuta ndani ya ndege inatoka wapi ikiwa,katika anga ambayo ndege hii inatembea kuna oksijeni kidogo?'
Kwanza,kuna kitu watu wengi wameelewa vibaya kuhusu upungufu wa oksijeni katika anga za juu....
SI KWELI KWAMBA OKSIJENI HUISHA NDEGE AU ROKETI INAPOPANDA JUU, NA NDIO MAAANA MFUMO WA KUTENGENEZA OKSIJENI NDANI YA NDEGE UNAHITAJIKA!!!
Kianchobadilika/kupungua ni mgandamizo wa hewa ya oksijeni (air pressure) na hilo hufanya iwe vigumu kwa mtu kupumua.
Hewa tunayovuta juu ya ardhi ina mgandamizo na unyevu-nyevu mkubwa na hii inasaidia pia kuweka mapafu na njia za hewa katika hali salama...kwa nini?
Ni kwa sababu katika matundu ya pua kuna ute-ute uitwao Mucus,unaosaidia kunasa bacteria na kuwazuia
kuingia katika miili yetu na kusababisha magonjwa.
Hewa iliyopo ndani ya ndege ni kavu na nyepesi,kwa sababu ipo chini ya mgandamizo (pressure) lakini haina unyevu-nyevu.
Hii ni kwa sababu hewa hiyo INATOKA KWENYE INJINI ZA NDEGE!
Kama ulisoma makala katika ukurasa wa blog hii kwenye Facebook http://facebook.com/Runway29R
uliona jinsi injini ya ndege inavyofanya kazi. Kwenye sahemu ya injini ambayo inagandamiza hewa (engine compressor) na kuipeleka kwenye sahemu ya kuchanganya mafuta na hewa na kuchoma mchanganyiko huo na kutengeneza nguvu,ndipo hewa inayotumiwa na abiria inapotoka.
Kutoka huko,kuna mfumo unaitwa Bleed Air system unaochukua hewa kutoka kwenye injini na kuuingiza kwenye chumba cha abiria.
Unakumbuka tulisema hewa iliyopo ndani ya ndege haina unyevu-nyevu na ni kavu? Na pia jinsi hewa tunayovuta ardhini (yenye unyevu-nyevu) inavyotusaidia kujikinga na magonjwa?
Kama unakumbuka,unaweza kujiuliza "Si ni rahisi sasa kama kuna abiria ana ugonjwa unaoambukizwa kwa njia ya hewa,kuwaambukiza abiria wengine?"
Jambo hilo limetiliwa mkazo sana na mainjinia wa ndege na ndio maana wametengeneza mifumo ya kuua vijidudu vya magonjwa. Wametengeneza mfumo ambao unaosafisha hewa ndani ya ndege kabla hata ya hewa hiyo kukufikia abiria. Juu ya kila kichwa cha abiria au kwenye miguu,kuna button mbalimbali pamoja na tundu lenye kitu kama nyavu. Linaitwa AIRCRAFT CABIN AIR FILTER.
Ndani ya tundu hilo kuna huo mfumo unaosafisha hewa kabla ya kuja kwa mtumiaji/abiria kama ionekanavyo kwenye picha...
Hivyo,usiwe na wasiwasi kwamba unaweza kupata magonjwa yoyote ukiwa ndani ya ndege.. Ni Salama Sana.