Feb 1, 2013

SHIRIKA LA NDEGE LA UINGEREZA BRITISH AIRWAYS KUSITISHA SAFARI ZAKE KUJA DAR ES SALAAM!

Shirika la ndege la Uingereza (British Airways) litasitisha rasmi safari zake za moja kwa moja toka London Heathrow Uingereza ifikapo Machi 1.

Hazijatajwa sababu za kufanya hivyo,lakini inaonekana ni kwa sababu ya soko la wateja. Kuna mashirika mengi yenye safari kama zake (safari za moja kwa moja toka Uingereza).
Abiria wanaokuja Tanzania kwa kutumaia British Airways watapitia Nairobi Kenya au Johannesburg Afrika Kusini. Mashirika kama vile Precision Air services,Kenya Airways,South African Airways na KLM Royal Dutch Airlines yatatumiwa na British Airways kusafirisha abiria wanaokuja Tanzania toka Nairobi na Johannesburg.

Mashirika kama Qatar Airways ndio yanayosemekana kuharibu soko la British Airways,kwa sababu linatoa huduma nzuri na lina wateja wengi!